Usajili wa wachezaji soka Ulaya
Hapa utaona dondoo za usajili kutoka maeneo mbalimbali Ulaya.
Arsenal inachuana na Manchester United katika harakati za kumsajili kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante (31).
Arsenal iko kwenye mazungumzo na Benfica baada ya kupeleka ofa ya £6.4m kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto mhispania Alex Grimaldo (26).
Chelsea wanajiandaa kukubaliana na ada wanayotaka Napoli ya £34m kwa ajili ya mlinzi wake wa kati raia wa Senegal Kalidou Koulibaly (31).
Bayern Munich inamsaka mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane (28) kama mbadala wa Robert Lewandowski (33) kutoka Poland anayetaka kuachana na mabingwa hao wa Bundesliga msimu huu.
Chelsea na Paris St-Germain nazo zitaingia kwenye mbio za kutaka saini ya Lewandowski kama itashindikana kujiunga na Barcelona.
Barcelona wanaamini watamsajili kiungo mreno Bernardo Silva (27) kutoka Manchester City.
Labels: Sports