Waziri Mkuu Uingereza ajiuzulu
Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative.
London. Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative.
Boris amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Julai 7, 2022 lakini bado atabaki kuwa Waziri Mkuu mapaka chama hicho kitakapopata kiongozi mpya mwezi Oktoba.
Katika hotuba yake, Boris amesema “Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani. Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’
"Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’
Amejiuzulu baada ya kuhudumu katika wadhifa huo chini ya miaka mitatu, licha ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa 2019.
Kinachofuatia baada ya kiongozi huyo wa Conservative kujiuzulu, uchaguzi wa kiongozi mpya wa chama unaanzishwa ambapo chini ya sheria za sasa, wagombea wanahitaji kuungwa mkono na wabunge wanane wa chama hicho ili kuwania.
#Soma zaidi HAPA
Labels: News
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home