Friday, 8 July 2022

Sepp Blatter na Michel Platini wafutiwa mashtaka ya ulaghai na mahakama ya Uswizi

Sepp Blatter na Michel Platini wafutiwa mashtaka ya ulaghai na mahakama ya Uswizi.

  • Wawili hao waliachiliwa huru kwa shtuma ya kufanya malipo ya faranga za Uswizi milioni 2 yaliyofanywa mwaka 2011.
  • Malipo yaliyofanywa kwa Platini kwa huduma za ushauri za Fifa.


Sepp Blatter na Michel Platini wamefutiwa mashtaka ya ulaghai katika mahakama ya Uswizi. 


Wanaume hao wawili, waliokuwa miongoni mwa vigogo wa soka, waliachiliwa huru kwa kupanga malipo ya faranga milioni mbili za Uswizi (£1.7m) kinyume cha sheria mwaka 2011. Wakati huo, Platini alikuwa rais wa Uefa na makamu wa rais wa Fifa na alitarajiwa kumrithi Blatter kama rais wa Fifa, shirikisho la soka duniani.


Malipo kwa Platini kwa huduma za ushauri katika muhula wa kwanza wa Blatter kama rais, kuanzia 1998 hadi 2002, yaliidhinishwa na Blatter Januari 2011 lakini yakaishia kumaliza kazi za wanaume katika soka.


 Waendesha mashtaka wa Uswizi walikuwa wameiambia mahakama huko Bellinzona kwamba "ilifanyika bila msingi wa kisheria" na "ilimtajirisha Platini isivyo halali" lakini hakimu katika kesi yao aliwakuta hawana hatia. Platini sasa atarejeshewa CHF 2m yake. 


Kamati ya maadili ya Fifa ilikuwa imewapiga marufuku kujihusisha na soka na kuwaondoa madarakani, na Blatter na Platini walipeleka kesi zao kwa kamati ya rufaa ya Fifa bila mafanikio na baadaye katika rufaa tofauti kwa mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo.


#soma zaidi HAPA


Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home