Wednesday, 16 May 2018

City Wamebeba Ubingwa Lakini United Watapewa Pesa Nyingi


City Wamebeba Ubingwa Lakini United Watapewa Pesa Nyingi Kuliko Wao, Sababu ni hii


Msimu wa EPL 2017/2018 umekwisha rasmi siku ya Jumapili tarehe 13/5, na mabingwa wameshapatikana ni Manchester City huku pia timu zinazoshuka daraja zimeshajulikana ni Stoke City, Swansea na West Bromwich Albion.

Kushinda kwa Manchester City kunamaanisha watapewa £153.2m kutoka EPL, pesa hizi ni kutokana na namna ambavyo mechi zao zimerushwa na pia kuna kiasi cha pesa ambacho timu zote za EPL hupewa.

Iko hivi City kama bingwa anapewa £39.8m kutoka Epl, lakini pia kuna hii pesa ambayo kila timu wanapewa kiasi sawa(equal share) ambapo huwa ni £82m, pia kuna pesa kutokana na idadi ya mechi zako zilizooneshwa live(haki kutoka Epl) na hii walitakiwa kulipwa £31.5m, jumla ya pesa zote hizi ni £153.2m.

Sasa linapokuja suala la United wao japo wamemaliza nafasi ya pili lakini watapewa pesa kuliko bingwa, United watapokea £153.6 kwanini? Baasi ni hivi United wanapokea kama kawaida equal share ya £82m, wakati City anapokea £39.8m za ubingwa, United wanapokea £37.8m ya mshindi wa pili, lakini United mechi zao ambazo EPL walirusha hewani live ni mechi mbili zaidi ya City na hii imewapa £33.9m katika mechi hizo na hapa ndipo walipowaacha City.

Suala hili lipo pia kwa mshindi wa 3 na wa 4, Tottenham amemaliza ligi katika nafasi ya 3 lakini jumla ya pesa ambayo wamevuna ni kiasi cha £148.1m, hii ni pesa ndogo kuliko ambayo Liverpool ambao wamemaliza ligi katika nafasi ya 4 wamevuna, Liverpool wamepata £149.6m na hii ni kutokana na mechi zilizoenda live.

Vilabu vilivyoshuka daraja navyo sii haba kwani wameshuka na fungu kubwa la pesa, Swansea amevuna £100m, West Bromich wakiweka mfukoni kiasi cha £98.5m sawa na mshindi wa mwisho Stoke City na hii imechagizwa sana na hii pesa £82.0m ambayo EPL wamekuwa wakitoa kwa kila timu.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home