Wednesday, 16 May 2018

Alikiba Apokea Tuzo ya Nyota wa Michezo



Ikiwa ni siku sita zimepita tangu Alikiba aachie ngoma yake mpya ‘Mvumo wa Radi’ amepokea tuzo ya heshima ya Plaque inayoitwa Nyota wa Mchezo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM.

Msanii huyo amepewa tuzo hiyo juzi Jumatatu kutokana na mchango wake kwenye muziki na jitihada alizopiga kupeperusha bendera ya Tanzania na ku-wainspire wasanii wengine wachanga na kuendelea kuwepo mpaka leo kwenye muziki.

Kiba amekuwa msanii wa tatu kupewa tuzo hiyo baada ya Vanessa Mdee aliyekabidhiwa mwezi January mwaka huu na Diamond aliyepewa mwezi wa tatu.

Kwa sasa video ya ngoma yake mpya ya Mvumo wa Radi ina views milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home