Tuesday, 17 April 2018

Diamond Platnumz Amefikishwa Polisi Kisa Video Zisizo na Maadili




BUNGENI: Msanii Naseeb Abdul Maarufu kama Diamond Platnumz amefikishwa Polisi jana kuhojiwa kutokana na kusambaza kwa video zake zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa Bungeni wakati akijibu swali juu ya kanuni za maudhi ya Mitandaoni

Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema Msanii Faustina Charles (Nandy) naye atahojiwa na Polisi kufuatia video yake ya faragha akiwa na Msanii mwenzake Billnas kusambaa mitandaoni.

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home