Barcelona na Man City waoneshwa mlango wa kutokea Champions League
Liverpool wakaibuka kidedea cha mabao 1-2 dhidi ya Man City na sasa Jurgen Klopp anakuwa kocha wa kwanza kuwahi kumfunga Pep Gurdiola michezo 3 katika msimu mmoja wa ligi na hiki kikiwa kipigo cha 3 kwa City mfululizo.
Habari kubwa ilikuwa nchini Italia ambapo As Roma wamefanya kile ambacho wengi hawakukitarajia baada ya kuitupa Barcelona nje ya michuano ya Champions League msimu huu, mara ya mwisho kwa Barca kupita katika hatua hii ilikuwa mwaka 2015.
As Roma wanakuwa timu ya 3 katika historia ya michuano ya Champions League kuwahi kupindua matokeo ya bao 3 katika mechi ya kwanza ambapo mwanzo timu mbili tu Deportivo la Coruna vs Ac Milan na Barcelona vs PSG walifanya hivyo.
Labels: Sports
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home