Mayweather Kuinunua Timu ya Newcastle na Kumsajili Ronaldo
![]() |
Mayweather ambaye ni bondia machachari awapo ndani na nje ya ulingo na anayetamba zaidi kuwa na fedha za kutosha amesema kuwa anafikiria kufanya uwekezaji katika soka.
Klabu ya Newcastle imekuwa kwenye harakati za kupata mmiliki mpya baada ya Mike Ashley kusemekana kuvunja mazungumzo kati yake na Amanda Staveley ya kuinunua timu hiyo.
Ni vyema ukaamini kuwa ningeweza kuwekeza, ningekuwa na kwenda mara kwa mara bondia huyo amekieleza chombo cha habari cha the Star siku ya Jumapili.
Nimekutana na baadhi ya wachezaji wa Newcastle mwaka jana, niwatu wema. Siku zote naanzisha nafasi za biashara na napenda michezo yote lakini nawekeza kutokana na kichwa changu kinavyonituma na siyo kutoka moyoni.
Kuwekeza kutoka ndani ya moyo ni rahisi kupata hasara lakini mtu akijitokeza na kushirikiana katika mipango ya kibiashara ni rahisi kutengeneza fedha, hivyo ningependa kuwekeza katika soka hatakama siyo mchezo wangu kwakuwa nina watu kila sehemu.
Labels: Sports
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home