Friday, 20 April 2018

Zitto: Serikali Inasema Uongo

Zitto: Serikali Inasema Uongo, Ni Muhimu Bunge Lichunguze Ziliko 1.5 Trilioni


Taarifa Ndogo ya ACT Wazalendo Juu ya Majibu ya Serikali Bungeni Juu ya Ziliko 1.5 Trilioni Zisizoonekana Matumizi yake Kwenye Ripoti ya CAG

Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Ni maelezo yale yale aliyoyatoa Katibu Mwenezi Taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu.

Kwa sasa tuna machache tu ya kueleza:

1.Serikali imesema uongo. Taarifa ya Serikali ya leo na Taarifa ya Fedha ya Benki Kuu, wanaotunza Fedha za Serikali hazisomani kabisa. Tutaongea na waandishi kueleza hili kwa undani zaidi. Ijulikane tu kuwa akaunti za Serikali kwenye Taarifa za Fedha za Benki Kuu hazina hizo Fedha Naibu Waziri ametaja.

2.Ni dhahiri kuwa kuwa ubadhirifu mkubwa wa Fedha za Umma, ndio maana taharuki ya Serikali ni kubwa, kiasi cha majibu ya Serikali kupewa Kiongozi wa CCM kuyasema, na kwa kuwa kashindwa kukonga nyoyo, sasa imebidi Serikali ije yenyewe kuyasema majibu yale yale yaliyosemwa na CCM. 

Tunashuhudia Kwa mara ya kwanza Zanzibar ikikusanyiwa zaidi ya TZS bilioni 200 Sawa na 20% ya Bajeti nzima ya Zanzibar, makusanyo yote ya TRA Zanzibar na mara 10 ya makusanyo ya Zanzibar kutoka PAYE za Muungano ambazo ndio pekee hukusanywa na TRA. Uongo huu wa Serikali ya CCM lazima unasukumwa na Wizi. Zanzibar hukusanyiwa TZS bilioni 21 tu na TRA, 200B zatoka wapi? Balaa

3.Sisi ACT Wazalendo, tunaendelea kumsihi Spika wa Bunge aruhusu Ukaguzi Maalum wa matumizi ya Shilingi 1.5 trilioni kupitia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, kwani hata haya majibu ya Serikali yanapaswa kuhakikiwa kwanza na CAG kabla ya kusomwa Bungeni, jambo ambalo halikufanyika. PAC wanajua kuwa makusanyo ya Serikali ni CASH BASIS na sio accrual. Serikali imedanganya, lazima PAC sasa wafanye kazi yao.

Muhimu: Tamko la Serikali ni matusi Kwa CAG. Watanzania mjiandae kuilinda Taasisi ya Ukaguzi wa Taifa. Serikali ya CCM inataka kuivunja vunja taasisi hii ya uwajibikaji. Tusikubali.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Aprili 20/2018


Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home