Taifa stars yaonyesha ubabe dhidi ya Congo DRC
Mchezo uliochezwa leo kati ya Taifa Stars dhidi ya Congo DRC umemalizika huku Taifa stars ikiibuka kidedea wa mechi hiyo kwa magoli 2 huku wageni wakiambulia nunge. Magoli hayo ya Taifa Stars yamefungwa na Mchezaji wa kimataifa anayechezea klabu ya KRC Genk nchini Ubelgiji Mbwana Samata akipachika bao la kwanza safi huku assist ikitokea kwa Kiungo mshambuliaji wa Club ya Simba nchini Tanzania Shiza Ramadhani Kichuya. Bao la pili lilipachikwa kimyani na Shiza Kichuya huku pass ikitokea kwa Mbwana Samata.
Labels: Sports
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home