Enzi Zetu
Watoto Wa Siku Hizi Hawajui Kabisa Enzi Zetu Unaweza Kuchapwa Kwa Sababu Zifuatazo:
![]() |
2. Umechapwa hukulia utachapwa tena
3. Ukijililia tu bila kupigwa, utachapwa
4. Kusimama wakati wazee wameketi, utachapwa
5. Ukiketi wakati wazee wamesimama. utachapwa
6. Kujipitishapitisha mahali ambapo wazee wamekaa, utachapwa .
7. Kuwajibujibu watu wazima, utachapwa
8. Usipomjibu mtu mzima, utachapwa
9. Kujifanya sugu wakati wa unachapwa, utaendelea kuchapwa.
10. Ukitoka kuchapwa, ukaimba au kupiga mruzi, utachapwa tena.
11. Usiposalimia wageni, utachapwa
12. Ukila chakula cha wageni, utachapwa.
13. Kuwalilia wageni wanapo ondoka, utachapwa.
14. Ukikataa kula, utachapwa.
15. Kuchelewa kurudi nyumbani baada ya jua kutua, utachapwa
16. Kula nyumba ya jirani, utachapwa.
17. Kujitia kisirani, utachapwa.
18. Kujitia kujuwa juwa sana, utachapwa.
19. Ukipigana na mtoto mwenzio, akakupiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
20. Ukipigana na mtoto mwenzio, ukampiga ukirudi nyumbani, utachapwa.
21. Ukiwa unakula chakula polepole, utachapwa.
22. Ukiwa unakula haraka haraka, utachapwa.
23. Ukiwa unakula sana, utachapwa.
24. Kuendelea kulala wakati wazee wamesha amka tayari, utachapwa.
25. Ukiwa unawaangalia wageni wakati wanakula, utachapwa.
26. Ukitembea na mtu mzima, ukajikwaa na ukaanguka, utachapwa.
27. Ukitembea na mtu mzima, akajikwaa ukamcheka, utachapwa.
28. Ukijamba mbele ya wakubwa, utachapwa.
29. Mtu mzima akijamba, ukamwangalia, utachapwa.
30. Ukila na wakubwa ukachukua nyama bila kupewa, utachapwa.
31. Ukinawa kabla ya wakubwa, utachapwa.
32. Ukimaliza kula ukanyanyuka kabla ya wakubwa, utachapwa.
33. Umechelewa kurudi dukani, utachapwa.
Kama umepitia malezi haya na bado ukakosa heshima basi wewe ni KONKODI
Maoni ya wadau
Mnanka: Ukiongea uongo, Utachapwa na Pia ukiwa mkweli kusemasema kila jambo utachapwa..
Humble: Ukiwa unaficha ficha siri utachapwaa
Ukiwa unasema sema tu hufichi siri napo utachapwaa
Mnanka: Ukiwa mchoyo, utachapwa
ukiwa mtoaji mtoaji wa vitu pia, Unachapwa..
Humble: Ukiitwa na mgeni mpitaji ukakataa utachapwaa
Ukiwa unaitwa na kila mpita njiaa unajipeleka tu napo utachapwaa
Mnanka: Ukizubaazubaa, Utachapwa na ukiwa mjanja mjanja, Utachapwa
Humble: Wakati wa kula ukiwa humalizi chakulaa utachapwaa
Ukimaliza chakula ukalamba sahani napo utachapwaa
Humble: Hizi adhabu zake nyingi hua makwenzii
Mnanka: Kuwahi kulala kabla ya chakula cha usku, utachapwa, kuchelewa kulala baada ya menu la usku, utachapwa.
Nakioze: Sijui kama watoto wa siku hizi hii wanaipitia
Humble: Watoto wa benteni hawaa hamnaa kituu
Mnanka: hii adhabu ni applicable pia..
Pale unapomdanganya mzazi na akaubaini ukweli halisi..
Au
ukaamua kusema ukweli halisi na akauthibitisha.
Humble: All way round utapigwaa hakuna afadhalii
Yaani adhabu yako inaamuliwa kabla ya kesho
Mnanka: Mie Mama yangu alikuwa ananichosha...
Ukifanya kosa, kabla hata Hajaskiliz maelezo, Unachapwa na ukishatoa maelezo, Unachapwa.
Ukijidanganya usitoe maelezo apo ndio kichapo cha Non-stop
Humble: Hahaha yaani hapo kitakacho kuponya ni kutoa ushirikiano kamilifu na kuweka sura ya huruma huku ukilia barabara ili upunguze idadi ya viboko
Humble: Maana lazima uchezee
Nakioze: Maana jana Geita tetemeko limepita mida ya saa sita usiku Baba mwenye nyumba kakurupuka toka ndani mwake kuangalia ni nini kufika sebuleni kakuta wanawe wanacheki indian movie daah
Nakioze: Sasa baba analala kabla ya wanawe hali hii ni ya kisasa zaidi
Mnanka: huu ndio usasa mnaoutaka... Baba anaingia kulala saa 4, watoto saa 7.
Zamani baba akigonga mlango tunahamisha Channel haraka kwenda TVT (TBC kwa sasa)
Lakini leo madogo wanaweka channel wanayoitaka afu wanatoa betri kwenye Rimoti.
Stay tune for the next episode ndani ya Opinions za Wadau
Labels: Opinions
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home