MAISHA HATIMAYE: DAY 1
Huu ni muhtsari wa mahubiri ya MAISHA HATIMAYE yanayoendelea Jijini Mbeya pia yanarushwa live kupitia Morning Star Tv na Radio yakiletwa kwenu na Chama cha Wajasiriamali na Wanataaluma Waadventista nchini Tanzania (ATAPE) huku mnenaji akiwa ni Makamu wa Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana toka nchini Marekani.
KISIMA KISICHOKAUKA: MUNGU NI MKUU
- Haya ya Maji na kiu inapotokea hutaabisha sana. Na ikiwa hakuna maji kiu hutaabisha.
- Uhaba wa Maji ni dhiki, taabu na pia ni kiu mbaya.
- Ikiwa hata kuna kiu Kali, lakini kuna kisima cha Maji Kisicho kauka.. Maisha huwa ni mazuri
- Pengine umepitia ukame na Jangwa katika maisha na unatafuta njia pekee ya Kutoka katika taabu yako(kiu yako).. Leo kipo kisima kisicho kauka.
- Ukikipata na ukakitumia kwa makusudi Yaliyowekwa utashuhudia Makubwa Kwa Maisha Yako. Na hautaona kiu Tena.
ZABURI 36:9
- Maana Kwako wewe iko chemchemi Ya Uzima. Ambayo Ni Mungu Pekee aliye Chemchem Ya Uzima.
- Yesu amegusa maisha yako na ameugusa moyo wako leo ione chemchem ya uzima.
- Kuna watu wanatembea wakiwa wamekufa na hawaoni badiliko lolote katika maisha, wanahitaji uzima.
- Yesu Ndiye awezaye kukifunua kisima cha uzima ndani yetu na maji yakabubujika ndani Ya mioyo Yetu.
- Mungu Ni Mkuu Mno, ana majina mengi sana maana na yanatumika haya mengi kwa Sababu Ya sifa zake.
- Wakati Mwingine tumemfanyia matani, tukamshusha kwa ngazi zetu za Kibinadamu tukamuweka kwa viwango vya chini sana...lakini Leo nakutangazia MUNGU NI MKUU MNO
YEREMIA 10:6
- Wewe Mungu ni Mkuu Mno, Jina Lako Ni Kuu, Wewe mwenyewe ni mkuu na Mungu wako Ni Mkuu.
1 Nyakati 16:5
- Hakuna Mungu Kama wewe, hakuna wa kulinganishwa kama wewe
- Muache Mungu aitwe Mungu, na Ni Mkuu katika Mambo Haya;
1) UMBILE LAKE - Halielezeki
2) UWEZO
3) SIFA ZAKE (Ni hizi) nazo ni za peke Yake
- KWA MAMLAKA
- NI WA MILELE
- ANAJUA YOTE
- HABADILIKI BADILIKI
- NDIYE MWENYE UWEZA WOTE
- SI WA KUFANYIWA MZAHA
- NI WA KUTISHA TENA SANA
- NI MUNGU MWENYE UPENDO, MPOLE, REHEMA, MVUMILIVU, FADHILI.
" ANASHUKA AINGIE KATIKA MAISHA YAKO."
Anashuka Ili Akupandishe Juu akuweke Kifuani Mwake, Mkaribishe akubariki na kukuweka kifuani mwake. Akishuka mpokee, mkaribishe na mpe Nafasi.
Mwanzo 28:15
- Mungu huyu aliye Mkuu anajali Sana Maisha Yako, anakufaham na anajua kila kitu kuhusu wewe.
- Tazama mimi nipo pamoja nawe Leo Hii Tambua..UPO KWENYE UWEZA WA MUNGU....
- Anatembea pamoja na wewe ukimkubali, na ukimkataa anatembea pembeni yako anakulinda na kukuwekea Ulinzi.
- MUNGU ANAKUPENDA YUKO MAISHA MWAKO NA ANANGOJA UWEKE MAHUSIANO YA DHATI PAMOJA NAE..
Ayubu 22:11
- Kama tunataka mema maishani mwetu, MJUE SANA MUNGU, MEMA YATAKUTOKEA.
- Mtafute anapatikana, mchunguuze utamuona na mtafakari atakutokea. MUNGU WETU NI MKUU
ISAYA 40:26
- Mungu ni Mkuu anajua majina ya kila nyota.. Ni ukuu wa namna gani Huu...ajabu sana Mungu wetu Ni Mkuu...mamilioni ya Nyota aliyaumba na kuyawekea namna ya mzunguko wake. Na ajabu anaziita kwa majina.
Msaada wangu utatoka wapi? Unapatikana kwa Mungu Pekee, Mkabidhi Maisha Yako Leo.
Wimbo: Namba 7: Mungu Msaada Wetu
BWANA AKUBARIKI SANA.
Imeandaliwa na;
MALIMA, K.
MALIMA, K.
Labels: FAITH
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home