Zitto: Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji
Zitto: Nitampeleka Abdul Nondo Uhamiaji
![]() |
| Haki miliki ya picha NONDO FACEBOOK/ KABWE TWITTER Image caption Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Mjini, Jimbo analotoka Abdul Nondo |
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema atamsindikiza kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo katika makao makuu ya uhamiaji Tanzania.
Angalia ujumbe wa Facebook wa Zitto
Mwisho wa ujumbe wa Facebook wa Zitto
Hii ni baada ya taarifa iliotoka kutoka mtandao huo ambao ulieleza kuwa Bw Nondo alipata barua ya kuitwa na uhamiaji ili 'akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake.'
Taarifa hizo zilisema 'afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake. Na kuwa wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo,hivyo awathibitishie kuwa yeye ni Raia wa Tanzania.'

Angalia ujumbe 2 wa Facebook wa Zitto
Mwisho wa ujumbe 2 wa Facebook wa Zitto
Abdul Nondo anashatakiwa kwa kosa la kudanganya kuwa alitekwa na kudaiwa kutoa taarifa za uongo mtandaoni.
Abdul Nondo apandishwa kizimbani Tanzania
Wanafunzi Tanzania hawaamini uchunguzi wa Polisi
Marekani: Tunasikitishwa na vitendo vya utekaji na ukatili Tanzania
Taarifa za kupotea kwa Bwana Nondo katika mazingira ya kutatanisha ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.
Hali hiyo ilipeleka taharuki miongoni mwa wanafunzi wenzake na jamii kwa ujumla huku wengi wakidhani kuwa bwana Nondo alikuwa ametekwa.
Sasa Bw Nondo anatakiwa kurudi uhamiaji tarehe 20 mwezi Aprili na 'kupeleka cheti chake cha kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa cha baba yake, mama yake, cha bibi na babu mzaa baba na mzaa mama.
Source: BBC Swahili
Labels: News

0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home