Waithiopia Watinga Nchini Kwaajili ya Mechi yao na Yanga
![]() |
Welayta imetua na kikosi chake kamili kilichoiondoa Zamalek ya Misri kwenye michuano hiyo hatua ya kwanza na wachezaji wakionekana kuwa na morali kubwa kuelekea mchezo huo.
Timu hiyo inashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi ya nchini kwao ikiwa na alama 23 katika mechi 17. Mchezo unatarajia kupigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam April 7.
Kwa upande wa Yanga yenyewe imeweka kambi mkoani Morogoro kwaajili ya mchezo huo na itarejea Dar es salaam kesho Alhamisi tayari kwa mchezo huo ambao kama itautumia vizuri itarahisisha kazi ugenini wiki mbili zijazo.
Labels: Sports
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home