Wednesday, 4 April 2018

Sheria 13 Za Mpira Wa Miguu Wakati Tukiwa Watoto



1. Dogo mnene lazima awe Golikipa.
2. Mwenye mpira ataamua nani acheze na nani asicheze.
3. Penati itatokea tu pale mchezaji akiumia sana na kutoka damu.
4. Mechi itaisha kama kila mchezaji atakua amechoka.
5. Hakuna free kick, kitu kama icho hakipo kwenye mechi zetu.
6. Hakuna Refa, mchezaji anaweza kuzunguka na mpira ata nyuma ya goli.
7. Ukichaguliwa mwishoni ujue uwezo wako ni mdogo kuliko watu wote uwanjani.
8. Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka, au kutungua mpira endapo utanasa kwenye mti uku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.
9. Mwenye mpira akikasirika, mechi ndo itakua imefika mwisho.
10. Inaruhusiwa kubadili golikipa kama penati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.,
11. Yule mtaalam wa soka huwa hakosi namba ata siku moja.
12. Mwenye mpira huwa hatolewi ata akicheza vibaya.
13. ...........

Maoni ya wadau:

* dah umenikumbusha mbali.

* Kama kuna fundi wa kucheza hajafika basi timu iko tayari kucheza pungufu ili kumsubiri au kuweka mtu yeyote ila kwa masharti tu kwamba jamaa akifika unatolewa na fundi anaingia.

* Timu moja mchezaji akiwa na viatu basi timu nyingine huongeza mchezaji ili kufidia, ina maana timu ya watu 7 mmoja akiwa na viatu basi hii ya wasio na viatu wanakuwa 8.

* Mtu akiumia hadi anatoka damu tunaweka michanga kwenye kidonda

* Wakakao anza kufungwa ndio watavua mashati au tisheti wabaki kifua wazi

* Kabla mpira haujaanza mtaambiwa hamna madochi(ndoso) na olewako upige dochi(ndoso) yani upati namba tena

* Mwenye mpra akiumia mtampa pole wachezaj wote

* Kigiza kikiingia ni muda wa rafu*


Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home