Yanga timu pekee iliyoshinda mechi nyingi ...
Yanga timu pekee iliyoshinda mechi nyingi mfululizo VPL hadi sasa
Kwa mujibu wa takwimu za michezo ya ligi kuu Tanzania bara (VPL) Yanga ndiyo timu pekee ambayo imeshinda mechi nyingi mfululizo kati ya timu tatu za juu zinazowania ubingwa wa ligi hadi sasa.
Yanga imeshinda mechi nane zilizopita mfululizo na kujikusanyia alama 24. Tangu Januari 21, 2018 iliposhinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, mabingwa hao mara tatu mfululizo wa VPL wameendelea kushinda mechi zao za ligi hadi Machi 12 walipoishinda Stand United kwa magoli 3-1.
Mara ya mwisho Yanga kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa ligi ilikuwa Januar 17, 2018 Mwadui ilipowalazimisha suluhu kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
- 21/01/2018 Ruvu Shooting 0-1 Yanga
- 27/01/2018 Azam 1-2 Yanga
- 03/02/2018 Lipuli 0-2 Yanga
- 06/02/2018 Yanga 4-0 Njombe Mji
- 14/02/2018 Yanga 4-1 Majimaji
- 18/02/2018 Ndanda 1-2 Yanga
- 09/03/2018 Yanga 3-0 Kager Sugar
- 12/03/2018 Yanga 3-1 Stand United Simba inafuata nyuma ya yanga, wekundu wa msimbazi wameshinda mechi tano mfululizo kati ya nane lakini imeshinda mechi sita kwa ujumla kati ya hizo nane (kuna mechi ambayo walishinda lakini haikuwa kwenye mfululizo wa mechi za ushindi) walijikuta wakilazimishwa sare mbili na timu za shinyanga (mwadui 2-2 simba, simba 3-3 stand united).
Vinara hao wa ligi hadi sasa wamefanikiwa kutengeneza alama 20 kati ya 24 ambazo walikuwa wakiziwania katika michezo nane iliyopita.
- 18/01/2018 Simba 4-0 Singida United
- 22/01/2018 Kagera Sugar 0-2 Simba
- 28/01/2018 Simba 4-0 Majimaji
- 04/02/2018 Ruvu Shooting 0-3 Simba
- 07/02/2018 Simba 1-0 Azam
- 15/02/2018 Mwadui 2-2 Simba
- 26/02/2018 Simba 5-0 Mbao
- 02/03/2018 Simba 3-3 Stand United
Katika michezo nane iliyopita, azam wamepata jumla ya pointi 14.
- 27/01/2018 Azam 1-2 Yanga
- 03/02/2018 Azam 3-1 Ndanda
- 07/02/2018 Simba 1-0 Azam
- 11/02/2018 Kagera Sugar 1-1 Azam
- 16/02/2018 Lipuli 0-0 Azam
- 03/03/2018 Azam 1-0 Singida United
- 08/03/2018 Azam 1-0 Mwadui
- 11/03/2018 Azam 2-1 Mbao
Labels: Sports
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home