Thursday, 8 March 2018

Wajue Waliogundua Umeme


Pata picha dunia ya leo kusiwe na umeme,Dunia ingekuaje? maisha yetu yangekuaje?,je watu wangetambua tabia za sayari nyingine huko anga za juu?Vipi tungezijua simu?Vipi tungetumia kompyuta,intaneti? ni wazi pangekuwa panaboa (bore) sana.
Katika ulimwengu wa sasa watu wengi sana wanatumia umeme katika kuendesha shughuli mbalimbali,na wengine hawawezi kufikiri katika maisha yao bila ya kuwapo kwa umeme.

Japo tunafahamu kuwa umeme ni nishati inayozalishwa na tabia asili ya mazingira ila iliwachukua miaka mingi sana binadamu kujua jinsi ya kuutumia umeme ili kuendesha vitu vingine mfano taa na injini.
Swali la kwamba 'nani aligundua umeme ?' limekuwa gumu kujibu kwa neno moja au kwa kumtaja mgunduzi mmoja,kwakuwa wagunduzi ni wengina kila mmoja alikuwa na umuhimu wake katika ugunduzi huo.Ugunduzi wa umeme ni historia ilio kubwa na 'vichwa' vingi vilitumika katika kukamilisha ugunduzi huu.

Angalau tu kwa ufupi,tuangazie wale walioshiriki katika ugunduzi huo japokuwa ilikuwa katika miaka tofauti.

Mambo ya mwanzo kabisa yaliofanyika ambapo matokeo yake ni haya tunayaona leo,mfano tunapiga pasi kwa kutumia umeme,mambo haya yaliohakikisha mafanikio katika ugunduzi uliokuja kufanyika miaka ya baadae na akina BENJAMIN FRANKLIN na wengine yalianza katika miaka ya 600 BC.

Benjamin Franklin 

THALES wa MILETUS, alikuwa ni mwanasayansi wa mwanzo kutambua uwepo wa umeme katika mazingira ya asili.THALES alitambua 'mbegu' ya umeme tuli (STATIC ELECTRICITY) na kupendekeza nadharia ambayo ilieleza "Kusugua manyoya kutafanya kitu kuvuta kingine (kuvutana)" hapa unaweza kuielewa vyema nadharia hii kwa kufanya jaribio lifuatalo wewe mwenyewe.
UTAHITAJI;
  • Kitana
  • Vipande vidogo vidogo vya karatasi
  • Na manyoya lakini kama hukuyapata unaweza kutumia nywele za kichwani kwako.
HATUA;
  • Sugua manyoya au nywele za kichwani kwako kwa kutumia kitana ulichonacho (fanya hivyo kwa muda wa kama dakika moja tu) baada ya hapo,gusia juu ya vile vipande vidogo vya karatasi 
MATOKEO
  • Matokeo yake utaona vipande vya karatasi vinaganda kwenye kitana kama vyuma vinavyoganda kwenye sumaku.

THALES wa MILETUS

Mwanasayansi WILLIAM GILBERT ndie mtu wa kwanza kutumia neno 'UMEME' ,hii ilikuwa katika miaka ya 1600.

WILLIAM GILBERT

Katika mwaka 1660 OTTO VON GUERICKE aligundua kifaa cha kuzalisha umeme tuli (STATIC ELECTRICITY) ,ugunduzi wa kifaa hiki uliofanywa na bwana GUERICKE ulipelekea kutambulika zaidi kwa tabia za umeme au kwa maneno mengine tunaweza kusema ugunduzi wake uliwafunua watu ufahamu zaidi juu ya UMEME.Miongoni mwa tabia/sifa za umeme zilizogundulika ni-
  • Umeme unaweza kupita ndani ya 'vaccuum'
  • Katika muktadha wa umeme,kuna vitu/materials ya aina mbili,moja ni vile vilivyo na tabia ya kuruhusu umeme kupita na vinginevyo ni vile ambavyo haviruhusu umeme kuppita yaani INSULATORS na CONDUCTORS.
OTTO VON GUERICKE

Katika karne ya 17,karne muhimu zaidi katika ugunduzi wa vitu mbalimbali ikiwemo umeme,mwaka 1729 mwanasayansi STEPHEN GRAY alichangia katika uelewa zaidi wa umeme kwa kugundua uendeshaji wa umeme,miaka nane (8) baadae CHARLES FRANCOIS DU FAY aligundua kuwa umeme unaweza kuwa na elements aidha CHANYA (+) au HASI (-).
Baadae sasa mwanasayansi BENJAMIN FRANKLIN na EBENEZER KINNERSLAY walitoa majina kwa elements za umeme za HASI na CHANYA.Ugunduzi wa electro-magnetic induction ulieleza wazi ni kwa namna gani umeme uliweza kufanya kazi.
Tokeo la picha la STEPHEN GRAY
STEPHEN GRAY

Kwenye suala la electromagnetism,MICHAEL FARADAY alikuwa mtu muhimu sana kwa kuwa aligundua kuwa 'kupitisha sumaku katikati ya koili ya waya (WIRE COIL) kungeweza kuzalisha umeme; ni huyu huyu FARADAY ndie aliegundua injini/mashine inayoendeshwa kwa kwa kutumia umeme,baadae aliweza kutengeneza GENERATOR na TRANSFOMA (TRANSFORMER).

Tokeo la picha la CHARLES FRANCOIS DU FAY
CHARLES FRANCOIS DU FAY

Katika kipindi cha mwaka 1745-1747 ni PETER VAN MUSSCHENBROEK aliegundua 'LAYDEN JAR' ambapo ilikuwa na uwezo wa kuhifadhi umeme (STATIC ELECTRICITY) na kutoa kwa wakati huohuo.

> WILLIAM BENJAMIN
Mwanasayansi huyu aliamini kuwa 'radi ni mfumo wa umeme'
katika kuamini kwake huko hakuishia hapo,mnamo JUNE 15 1752,FRANKLIN alifanya jaribio ambalo ni maarufu sana la kurusha kishada wakati wa radi kwa lengo la kuthibitisha kuwa RADI ni mfumo wa umeme.
Kishada hiko alikifunga kitu cha asili ya chuma akiwa na lengo la kama kweli RADI ni mfumo wa umeme basi utapita kupitia kitu hicho cha asili ya chuma na kumfikia .
Kama zilivyo fikra zake,umeme kutoka kwenye RADI ulisafiri kupitia chuma kile na mpaka kumfikia bwana BENJAMIN FRANKLIN na kumpiga shoti.

LAKINI mwaka 1747 HENRY CAVENDISH alitoa orodha ya vitu vinavyopitisha umeme yaani materials that are conductive to electricity.Tukio hili lilifuatiwa na bwana VOCTA ambae yeye aliweka bayana kuwa 'chemical reactions'zinaweza kutumika katika kuzalisha 'anodes' na 'cathodes'
Ugunduzi wa BALBU(bulb) za umeme uliofanywa na THOMAS EDISON ilikuwa ni hatua kubwa sana katika maendelao ya teknolojia,na ni ilikuwa ni hatua ilioitoa dunia kwenye kiza.

Katika kipindi cha karne ya 20,umeme uliwafikia watu duniani kote,ugunduzi uliofanywa na wanasyansi tofauti tofauti na wagunduzi wa umeme kama akina THOMAS EDISON,SAMUEL MORSE na NIKOLA TESLA uliibadilisha kabisa dunia,dunia ya sasa kuna injini/mashine zinazotumia umeme kufanya kazi ambazo mwanzo zilikuwa zikifanywa na binaadam.
Wakati wa uhai wa wagunduzi akina THOMAS EDISON na WESTINGHOUSE kulikuwa na mabishano kati yao,mabishano hayo yalikuwa ni juu ya aina ya umeme uliofaa kutumiwa,THOMAS EDISON alipendekeza kutumika kwa umeme wa DIRECT CURRENT(DC) na WESTINGHOUSE yeye alipendekeza kuttumika kwa ALTERNATING CURRENT (AC).
Ugunduzi wao umetuletea manufaa makubwa, hivi sasa mitambo inagunduliwa kurahisisha kazi mitambo hiyo inategemea umeme kujiendesha,na hata teknolojia na tafiti za anga za juu zinakuwa rahisi kutokana na kuwepo kwa umeme. Hivi sasa umeme wa DC na AC wote unatumika ila tu hutegemea na mahali unapohitajika.

Reference CLICK HERE




Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home