Mambo 21 aliyoyafanya Nyerere kwa watanzania ...
Mambo 21 aliyoyafanya Nyerere kwa watanzania kwa miaka 24 bila kutegemea msaada
Kwa uchache tu awamu ya kwanza serikali ya taifa letu iliyodumu kwa miaka 24 toka 1961 hadi 1985 iliasisi na kuyajenga yafuatayo ambayo leo hii toka 1985 mpaka 2016 baadhi yamekufa ama yanayumba.
Awamu ya kwanza ya viongozi makini iliasisi na ilijenga yafuatayo
1. Taifa maskini lenye kujiamini. Taifa lililoamini katika kujitegemea bila kuhitaji misaada toka nje.
2. Kilimo kama uti wa mgongo wa maisha ya mtanzania katika kujiletea kipato. Kama taifa, nchi iliishi kwa kutegemea kipato cha mazao ya biashara (kahawa, pamba, pareto, korosho, mkonge, chai, alizeti, kokoa, tumbaku, mawese, karafuu n.k. Tanzania ilijulikana katika masoko ya dunia kwa uzalishaji na usafirishaji wa mazao tajwa hapo juu na uchumi uliendeshwa kwa kilimo.
3. Mazao ya chakula yalizalishwa pia na yalijengewa uwezo wa kipembejeo kuwasaidia wakulima. Serikali iliamua kwa makusudi kuimarisha uzalishaji wa kikanda ulioleta tija. Mfano ni big 4 kanda ya kusini iliyokuwa ikizalisha mahindi kwa wingi na kulisha nchi nzima. Mikoa ya Rukwa Ruvuma Mbeya Iringa.
4. Viwanda vilijengwa ili viweze kuimarisha uchumi kwa kupata malighafi toka kwa mkulima na kuzitengeneza mali kabla ya kuuza soko la ndani na nje ya nchi. Viwanda hivyo ni pamoja na vya kusafisha pamba (mwanza na shinyanga) na kutengeza nguo (mwanza, musoma, dar es salaam). kubangua korosho (mtwara, lindi, dar es salaam, kibaha). Viwanda vya kutengeza bidhaa za viwandani (mang`ula, moshi). Viwanda vya kahawa moshi na bukoba. Viwanda vya cement tanga, dar es salaam na mbeya. Viwanda vy mbolea tanga na mbeya. Viwanda vya vyombo vya ndani na magunia morogoro. Viwanda vya tumbaku morogoro na tabora. kiwanda cha chuma tanga. Viwanda vya sabuni tanga Arusha Dar na Mwanza. Kiwanda matairi Arusha. Kiwanda cha sigara Dar. Kiwanda cha pombe Dar es salaam, Arusha na mwanza. Kiwanda cha mkonge Tanga. Kiwanda cha kukata almasi Iringa. Kiwanda cha karatasi na mbao iringa.
5. Viwanja vya ndege vya kimataifa vilijengwa Dar na Kilimanjaro. Pia viwanja vidogo vya mikoani vilijengwa kwa usafiri wa ndege ndogo.
6. Shirika la ndege la Tanzania lilikuwepo na boeng 3 na ndege ndogo kama fokkers zilizosafirisha abiria nusu ya mikoa ya nchi yetu.
7. Meli za kusafirisha abiria zilikuwepo kwenye bahari ya hindi kutoka dar kwenda lindi, mtwara, zanzibar na pemba. Pia ziwa victoria, tanganyika na nyasa.
8. Treni za kusafirisha abiria na mizigo kutoka dar kwenda kigoma, mwanza, moshi na mpanda. Pia treni kutoka tanga kwenda moshi zilifanya kazi. Bila kusahau TAZARA iliyosafirisha abiria na mizigo toka Dar, ifakara, makambako, mbeya mpka Zambia.
9. Shirika la nyumba lilikuwepo na likajenga nyumba nchi nzima.
10. Benki ilikuwepo na ilifika makao makuu yote ya wilaya.
11. Shirika la simu na posta lilikuwepo na lilifika wilaya zote.
12. Shirika la umeme lilikuwepo na lilifika makao makuu yote ya mikoa kwa kutumia genereta na gridi ya taifa. Ikiwemo kujengwa kwake kwa mabwawa ya Kuzalisha umeme mnayoyaona leo yale ya kidatu, nyumba ya mungu, hale pangani na mtera.
13. Majeshi yote kuyaendeleza na kuyajenga upya ndani ya nchi yetu na kuweka msingi wa nidhamu uliodumu leo bila kuwepo mapinduzi ya serikali.
14. Vyuo vya elimu ya juu kuasisiwa na kuendelezwa isipokuwa Dodoma University.
15. Hospitali kuu ya nchi na za mikoa, wilaya na vituo vya afya vijijini kuasisiwa na kuendelezwa. Huduma ya afya kutolewa bure nchi nzima.
16. Muungano wa Tanzania
17. Kuwaunganisha watanzania kwa lugha moja ya kiswahili.
18. Kutaifisha, kusimamia, kuziendeleza na kujenga shule za sekondari na msingi nchi nzima ili kuleta uwiano kwa watoto wa dini na kabila tofauti ndani ya nchi yetu. Si hivyo tu bali elimu ilikuwa bure kwa wote.
19. Kushauri nchi iwe na mfumo wa vyama vingi na wa uchumi huria kwa manufaa ya watanzania wote.
20. Hifadhi za taifa na mapori tengefu yalisimamiwa na kulindwa bila kuwepo kwa utalii wala ujangiri unaangamiza tembo wetu.
21. Madini hayakuchimbwa kama ilivyo sasa na alishauri yaachwe yachimbwe tukiwa na uwezo. Isipokuwa Almasi, chuma na makaa ya mawe ambayo yalichangia katika uchumi wa nchi.
WAPI TUNAELEKEA? Swali hili linakuja wakati ambapo taifa limeanza kuvuna raslimali nyingi zikiwemo madini kama vile dhahabu, tanzanites, gas, oil na urani. Si hivyo tu pia uwindaji wa wanyama pori, utalii na uwekezaji kutoka nje umepanuka na kuwa mkubwa bila ya mapato yake kuonyesha kuwajengea uwezo watu walio wengi kupata unafuu wa huduma muhimu kama elimu na afya.
Reference: Click Here
Labels: Facts


0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home