Fahamu aina ya Watu unaotakiwa Kuachana nao Maishani
Unakosa furaha katika maisha yako kutokana na mambo mbalimbali,ikwemo mazingira,hapa namaanisha watu wanaokuzunguka.Ustawi mzuri wa maisha yako hutegemea watu wanaokuzunguka,kama utazungukwa na watu wenye mawazo chanya kuna nafasi kubwa kwa wewe kuwa mwenye furaha kwa kuwa watakupa moyo wa kufanya bidii zaidi kwa kile unachofanya,na kama utazungukwa na watu wengi wenye mawazo hasi kuna nafasi kubwa ya wewe kufeli katika mipango ya kimaendeleo ya maisha yako na kukosa furaha kwa ujumla.
Ni muhimu kuwatambua watu wa aina mbalimbali wanaokuzunguka,ikiwamo wale watakaokuwa nawe bega kwa bega kipindi cha kupanda mbegu na wale wanaokuwa nawe kipindi cha mavuno yaani wale marafiki 'feki' wanaokuwa nawe wakati wa furaha tu.
Hapo chini tumekuandalia orodha ya aina ya watu wa kuwakwepa/kuachana nao katika maisha yako ili wewe ubaki mwenye furaha na mwenye kufanikiwa katika mipango yako,watu wa aina hii ni kuwapuuza tu na kusema kuwapuuza hatuna maana kuwachukia, la hasha, bali ni kujijali mwenyewe na ustawi wako zaidi maishani mwako kuliko shutma na na maneno ya watu wa aina hii.
MARAFIKI WANAFIKI
Rafiki ni mtu ambae unamtegemea na anaekutegemea kimsaada au kimawazo na kukufariji wakati unapokumbwa na janga au tatizo,rafiki ni kama bega la kuegemea pale unapojihisi dhaifu na mnyonge,unapokuwa na urafiki na mtu mnakuwa kama ndugu.
Kuna watu wanaojifanya kuwa marafiki zako lakini vichwani mwao wanakuona kama 'fursa' wakiona kuwa kama watakumbwa na tatizo wewe ndio utakuwa mtu pekee na muhimu kuwasaidia na mara nyingi marafiki wa namna hii wanakutafuta/kukumbuka pale wanapokuwa na matatizo yao lakini unapokumbwa na tatizo lako wao huwa mbali kabisa na kuona kama haliwahusu.Kwa sababu hii basi ni muhimu kuwa makini katika kuwachagua watu ambao unaona watakufaa katika kufanya nao urafiki
Ni vyema kuwafahamu ni akina nani watakushika mkono utakapoanguka na akina nani watasherehekea na kufurahi utakapoanguka.Marafiki wanafiki ni wale ambao wanajifanya wanakupenda na kukujali lakini mioyoni mwao wanachukia maendeleo yako hivyo kufanya mipango ya siri ya kukushauri kufanya vitu ambavyo wao wanajua hautafanikiwa na pindi utakapo'feli' watakucheka na kukutangaza,na marafiki hawa hawatakubali ufanikiwe NO MATTER WHAT!.
Watataka kukuona unaingia matatizoni kwa kufanya vitu visivyo sahihi na kukuangusha badala ya kukushika mkono wakati unaposhindwa maishani,huwa hawapo pale unapowahitaji na huwa na ahadi (promise) za uongo.KUWA MAKINI SANA NA WATU WA AINA HII.
WATU AMBAO SI WASAMEHEVU.
Hakuna mtu aliemkamilifu ulimwenguni.Hivyo sote tunafanya makosa,Hii haina maana mtu kukosa umakini katika utendaji wake,ila cha msingi ni kuhakikisha tunasahihisha makosa tunayoyafanya,tunajifunza kutokana na makosa hayo na kuhakikisha tunatafuta njia bora ya kuzuia kurudia kosa lile lile.
Hata hivyo kuna watu kwao huwa ni ngumu sana sana kuwasamehe wale waliowakosea,na hutumia makosa yako ya nyuma kuku'judge' (kukuhukumu).
Kama kuna watu wanatumia makosa yako ya nyuma kukuhukumu au kutumia makosa hayo kuhakikisha wanakuangusha kisa tu uliwahi kuwakosea huko nyuma na umefanya juhudi zote za kuwaomba radhi/msamaha na zimeshindikana,basi ni vyema kuachana nao kabisa katika maisha yako.
Tumia makosa yako uliowahi kuyatenda huko nyuma kama muongozo katika maisha yako ya sasa na kama muongozo katika mipango yako ya 'future'.Jaribu kuwa na mawazo chanya katika kila kosa unalofanya,kubali kosa na muombe msamaha uliemkosea,jifunze kutokana na kosa hilo na tafuta njia bora ambayo itahakikisha haurudii tena kufanya kosa kama hilo.
WABABE
Wababe wanayafanya maisha ya watu kuwa magumu na yasio na furaha (labda wawe upande wako),wanayapa vipaumbele mahitaji yao na hisia zao juu ya watu waliowazunguka,Wanatumia nguvu zao kuwatisha watu na kuathiri mawazo yako,watasema na kufanya kitu chochote kukufanya wewe ufanye vitu wanavyotaka.Wanakuathiri kimawazo kwa kukutisha ilimradi wapate kile wanachotaka pasina kujali athari zozote.
WATU WANAOTAMANI KUKUONA UNAKUWA KAMA FULANI.
Labda una sauti nzuri ya kuimba na una ndoto za kuwa muimbaji/mwanamuziki,watu wanakwambia ''tunapenda kukuona unaimba kama NANDY,au MAUA SAMA au RAYVANNY,ukiimba kama wao utapendeza kweli'' Hii si sahihi,Jivunie kwa jinsi ulivyo,Tengeneza utambulisho wako wewe kama wewe na usiwe 'kopi' (copy) ya mtu mwingine,hakuna kitu kizuri kama kujua watu wanaokuzunguka wanakukubali kwa jinsi ulivyo na sio jinsi wanataka au wanaona unaweza kuwa,kama wanakukubali na kukupenda inabidi wakubaliane na mawazo yako ya vile wewe unataka kuwa na wao wakukubali kwa namna hiyo hiyo na si vinginevyo.
Kwa bahati mbaya kuna watu wanakusistiza kuwa kama mtu fulani,wanasema 'utafanya vizuri au utapendeza ukiwa kama yule',hawa huwa hawaoni maendeleo yoyote yale unayofanya kuonesha jinsi ulivyo,wanaendelea kusistiza kuwa utafanya vizuri kama utakuwa kama fulani.Kati ya watu wote ni wewe pekee unaejua kipi kizuri kwako,maisha utayaona mazuri kama utachagua kuwa kama wewe unavyotaka na inapendeza zaid kuona watu wanaokuzunguka wanakukubali kwa jinsi ulivyo.Ukikutana na watu wa namna hii jaribu kuwaeleza namna wewe unafikiri au unapenda kuwa,wapo watakaokuelewa ila kwa wale wasiokuelewa ni vizuri kuachana nao na kuwapuuza (si kuwachukia).
WATU WAGUMU KUELEWANA NAO (KUWA RADHI NAO)
Wapo watu wagumu kuelewana nao (kuwa radhi nao),wakati mwingine ni vyema kukubali kuwa katu hautaweza kuwa radhi nao bila kujali jitihada zote unazofanya ili kuwa nao sawa kimaelewano toka mwanzo,
Katika maisha unaweza kukutana na watu ambao hawatakupenda,hawatakuheshimu wala kukubali kile unachofanya hata kikiwa kizuri kwao PASIPO NA SABABU YEYOTE YA MSINGI.
Kitu pekee cha busara cha kufanya katika hali kama hii ni wewe kuachana nao na kuwapuuza badala ya kuanza mivutano isio na msingi,ukiwa umeshajaribu kuwa na maelewano nao na jitihada hizo zimeshindikana basi usimalize nguvu zako kujaribu kuwashawishi zaidi na kuwafanya wakukubali,ila nguvu zako zielekeze katika kufanya mambo yako ya kimaendeleo,waache washuhudie maendeleo yako.
WEWE MWENYEWE (YOURSELF)!
Hakuna adui mbaya kama wewe mwenyewe.
Unaweza kujiuliza ni kivipi wewe mwenyewe ujifanyie uadui?,inawezekana?
Jibu ni ndio kwa wewe mwenyewe kujifanyia uadui tena uadui ulio mkubwa!,Uadui huu unaweza kujifanyia mwenyewe kwa kutojiamini na kujisthtumu mwenyewe kutokana na kutokuwa kama fulani au kutofanya vizuri kama fulani.
ACHA kujishtumu wewe mwenyewe,inawezekana usiwe kama watu wengine na usifanye vizuri kama watu wengine lakini kuna kitu cha pekee unacho ambacho wengine hawana.
Kila mmoja ni tofauti na mwingine na ndio maana unatakiwa UACHE kujishutumu wewe mwenyewe kwa kukosa au kutofanya vizuri katika jambo lolote,na pia acha kujilinganisha na wengine,Jikubali wewe mwenyewe na furahia kile ulichonacho.
USIFIKIRIE SANA KUHUSU VILE AMBAVYO HUNA/UMEKOSA NA BADALA YAKE FIKIRIA ZAIDI VITU AMBAVYO TAYARI UNAVYO.
Labels: RECALL
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home