Thursday, 15 March 2018

Balcelona Yaidhibu Chelsea Na Kuitoa Njee Ya Mashindano Ya Uefa Championi Ligi


Balcelona Yaidhibu Chelsea Na Kuitoa Njee Ya Mashindano Ya Uefa Championi Ligi
Club pekee iliyokuwa ikicheza Champions league kutoka jiji la London, usiku wa kuamkia leo imeyaaga mashindano hayo, shukrani za pekee ni kwa goli kipa wa Chelsea anayeitwa Courtouis kwa kuruhusu mabao yaliyowekwa kimyani na Mfalme wa soka King Lionel Messi pamoja na mchezaji kutoka Taifa la Ufaransa O.Dembele.

Mechi hii iliisha huku Barcelona wakiibuka na ushindi wa magoli 3-0 nunge dhidi ya wapinzani wao Chelsea.

King Leonel Messi akishangalia mabao yake mawili aliyoyafunga dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Nou Camp Catalunya.

O.Dembele winga ambae amechukua nafasi ya Neymar Jr nae pia jana hakuwa nyuma, kwani aliweza kupachika bao safi dhidi ya Chelsea kutoka Jijini London.


Mechi  nyingine iliocheza jana ni kati ya Besiktas kutoka nchini Uturuki vs Fc Bayern Munich kutoka nchini Ujerumani matokeo Bayern ilishinda bao 3-1 hivyo imefuzu kucheza mashindano hayo robo fainali.

Bayern Munich midfielder Thiago aliwapatia wageni goli la kwanza dhidi ya Besiktas nchini Uturuki kabla ya kutolewa nje sababu ya majeraha aliyoyapata baada ya dakika 35 ya mchezo hivyo nafasi yake ikachukuliwa na mchezaji mwenzie kutoka nchini Colombia James Rodriguez.






Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home