Monday, 12 March 2018

Baada ya Kula Kipigo Kikali Shilole Afunguka Mazito ...


Baada ya Kula Kipigo Kitakatifu Shilole Afunguka Mazito "Siku Moja Nitaongea Mazito na Kudai Talaka"

Msanii wa Bongo fleva Shilole amefunguka na kueleza chanzo cha kichapo kizito alichotembezewa na mumewe uchebe ambapo amedai kisa na mkasa ni yeye kucheza mziki na Soud Brown wa shilawadu kwenye sherehe.







"Tena Soudy niache kabisa wewe ndio umefanya mpaka mimi nagombana na mume wangu eti uchebe anasema wewe bwana wangu kweli? Eti siku ile kule Tabata tulivyokuwa tumekaa meza moja eti kakasirika tulivyokuwa tunacheza muziki kwahiyo ina maana mimi nisicheze na mashabiki eti! Mimi sitaki kuongea mambo mengine nikaonekana mkorofi wa ajabu" alisema shilole wakati akihojiwa na Soudy Brown wakati akihojiwa kwenye You Head.

Lakini Shilole alikiri kupigwa kama mtoto na Uchebe kiasi cha kufunga mtaa hadi kupelekea Shilole kwenda kulala kwa marafiki zake "Yaani Uchebe amenipiga kama mtoto lakini haoni noma mimi mwanamke wa dunia nzima kuna mambo mimi ntakuja kusema mazito alafu ndio nitadai talaka yangu"

Labels:

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home